SURA YA 2: Uhuru wa Uchumi na Amani
na Erik Gartzke
Utangulizi
Kwa
kuwepo kwa vita katika Mashariki ya Kati na kushamiri kwa mashambulizi
ya kigaidi katika maeneo kuanzia viwanja vya ndege vikubwa hadi eneo la
maduka, inafaa tujikumbushe kuwa sehemu kubwa ya dunia iko katika hali
nzuri ya amani kubwa. Hakika, nchi zilizoendelea hazijapigana tangu Vita Kuu vya Pili ya Dunia. Amani hii siyo ya kawaida kwa kuwa mataifa yenye nguvu kihistoria yalikuwa katika vita vya mara kwa mara. Hata kabla ya wakati wa Thucydides, serikali zilitumia mali kupata maeneo zaidi na kutawala mambo ya jirani zao. Kwa
kuelewa sababu kwamba nchi zenye nguvu za leo hazina migogoro sana kama
waliowatangulia ni vigumu kudumisha amani na kupanua zaidi manufaa yake. Sera
zilibashiri kuhusu uhusiano usio sahihi baina ya demokrasia na amani;
kwa mfano, zinaelekea kusababisha matatizo mengi kama wanavyoyatatua.
Nadharia
za kimapokeo zenye mtazamo usiojifunga zina mikondo miwili ya kuelezea
amani, mmoja unaolenga aina na shughuli za serikali, mwingine kuhusu
masoko huria na raslimali binafsi. Ya kwanza inaonekana
zaidi katika maandishi ya Immanuel Kant, imevuta usikivu mkubwa kutoka
kwa wafunzi wa siasa za kimataifa katika mwongo uliopita. Kant
alikosea alivyodai kuwa jamhuri sio za vita sana kama aina nyingine za
serikali, badala yake watafiti wamegundua kwamba nchi za kidemokrasia
hazina tabia ya kupigana wenyewe kwa wenyewe, na haziko tayari kwa
ujumla kutumia nguvu. “Amani hii ya kidemokrasia”
imepigwa marufuku kisheria kwa ugunduzi kwamba demokrasia zinazoendelea
zinaelekea kuwa za kivita kama udikteta unaoendelea. Maelezo
yaliyopo yanayohusu juhudi zenye amani za taratibu, taasisi za
kidemokrasia au kanuni za uwazi lazima zipambane kuelezea kwa nini
mafanikio ni sharti la amani.
Uchumi wa kisiasa wa mtazamo usiojifunga hauna tofauti hizo. Wasomi,
kama vile Montesquieu, Adam Smith, Richard Cobden, Norman Angell, Na
Richard Resecrance wamekisia kwa muda mrefu kwamba soko huria lina
nguvu kwa serikali huru kutoka kwenye matarajio yanayoonekana ya vita
vya mara kwa mara. Ubepari unahimiza ushirikiano miongoni mwa nchi kwa kutengeneza mazingira yanayoifanya vita isiruhusiwe au isiyokuwa ya lazima. Masoko
huria ni eneo lingine la ushindani miongoni mwa nchi mbalimbali, mara
nyingi migogoro ni midogo isiyohitaji utumiaji wa nguvu za kijeshi. Mageuzi ya bishara yaliyowezeshwa na uhuru wa uchumi yalipelekea pia katika mabadiliko ya masuala ya kimataifa. uvamizi unakuwa ghali na usio na faida. Utajiri katika uchumi wa kisasa ni mgumu sana ”kuiba” kwa kutumia nguvu kuliko ilivyokuwa kwa jamii za kilimo na za viwanda. “Amani
ya Kibepari” imekwenda na uthibitisho upo sasa kwa ajili ya kuanzisha
uhusiano imara zaidi baina ya uhuru wa uchumi na kupunguza migogoro. Ninatumia
kielelezo cha uhuru wa uchumi kilichotengenezwa na Gwartney na Lawson
na uchambuzi mwingi wa takwimu kuonyesha kwamba masoko huria yanaelekea
kuhimiza amani. Aidha ninatathmini vipengele kadhaa ambavyo mara kwa mara vimedhaniwa kuzifanya nchi zipigane. Uhuru wa uchumi ni mojawapo ya vipengele adimu ambavyo kwa kawaida vinazuia migogoro miongoni mwa mataifa.
Demokrasia
inafaa kwa sababu nyingi lakini sera zinazohimiza, au hata zinazotafuta
kuweka, serikali ya uwakilishi hazielekei kuchangia moja kwa moja
katika amani ya kimataifa. kama matokeo yaliyoripotiwa
hapa yalivyo wazi, masoko huria na si demokrasia, yana athari kubwa kwa
tabia ya nchi hadi kufikia vurugu za kijeshi. Sanasana, demokrasia, inaweza kupunguza migogoro tu miongoni mwa nchi zilizoendelea kiviwanda. Nchi zinazoendelea hazinufaiki na amani ya kidemokrasia. Hasa
katika majimbo yanayotawaliwa na serikali za kiautokratiki, uanzishwaji
wa demokrasia unaweza kuwa na athari ndogo za mara moja katika
ushirikiano wa kimataifa. Vivyo hivyo, utafiti mkubwa
unaonyesha kwamba serikali ya kidemokrasia ni imara tu inapochanganywa
na viwango vya hali ya juu vya maendeleo ya kiuchumi. Katika
kutenganisha, sera zilizobuniwa kwa ajili ya kuzifanya nchi
zinazoendelea kuwa za kidemokrasia haziwezi kuthibitisha ama uimara wa
kisiasa wala amani ya kimataifa. Kwa kuwa mafanikio ni ya
lazima kwa ajili ya kuwa na demokrasia imara na inayotosha kuleta
amani, sera ya nje iliyo bora ni ile ambayo inaendeleza na kukuza
ubepari.
Usuli
Wanafunzi wa uchumi wa siasa wa kimataifa wamehoji kwa muda mrefu kwamba masoko ya dunia yanaendeleza urafiki wa duniani. Cobden
aliita biashara “utatuzi mkubwa ambao kama ugunduzi wa ufadhili wa
tiba, utasaidia kukinga afya na kwa ajili ya kuokoa ustaarabu wa
mataifa yote ya dunia” (1903:36). Kant aliandika kuwa ipo siku ari ya biashara, ambayo hailinganishwi na vita, itashinda katika kila nchi” (1975:32). Mill
alidai kwamba “Ni biashara ambayo kwa haraka sana inaifanya biashara
kutokufaa, kwa kuimarisha na kuzidisha maslahi binafsi ambayo huupinga
kiasili” (1902: 390). Bila shaka tatizo, ni kwamba Mill alikosea. Vita
vingi na migogoro midogomidogo vinasimama baina ya msimamo wa kutegemea
mazuri wa sasa na wa zamani wa wachumi wa siasa ya msimamo wa
kupendelea mabadiliko wa karne ya kumi na tisa. Walipungukiwa na nini? Walielewa nini kwa usahihi? Wana ushahidi gani kwamba msingi wa dira yao una utambuzi wenye uhalali na kudumu?
Mawazo yanapungua na kufuatana na matukio ya sasa. Madai kwamba ubepari unaweza kuzifanya nchi kuwa na vita kidogo yanakuwepo kwa urahisi wakati masoko ni mengi na hakuna vita. Wanasiasa
weledi na wasomi wa karne ya kumi na tisa walijumuisha uhusiano baina
ya masoko huria na amani ya kimataifa, hatimaye kuiona Ulaya
ikigawanyika mwaka 1914. Vilevile, ni rahisi kutazama dunia kama za Hobbersian kwa ujumla wakati migogoro ya kiuchumi na kisiasa inapojitokeza. Wasomi
wanaangalia mambo kama yalivyo kama vile Kenneth Waltz na John
Mearsheimer wakati wa Vita Baridi walishikilia kwamba uhusiano wa
uchumi wa dunia haukudhuru sana uendeshaji wa masuala ya nchi, licha ya
uthibitisho kwamba mataifa huru na ya viwanda ya dunia hayakuwa ya
kivita sana. Uelewa madhubuti wa uhusiano wa kimataifa –
bila ya kuzungumzia utafutaji wa amani duniani – unadai kwamba nadharia
ni zaidi ya muhtasari wa mtindo wa kisomi. Duniani ni mahali pa makelele. Mara nyingi, kubuni yatakayotokea kutokana na matukio ya sasa kunatupotosha. Hakika, inaelekea zaidi
kwamba uhusiano baina ya uhuru wa uchumi na amani sio halisi lakini
badala ya uwezekano wa tukio la kijamii na kukabiliwa njia mbalimbali
za kupelekea katika vita. Kwa utumiaji wa uchambuzi wa
takwimu kwa siasa za dunia, tunaweza kwenda zaidi ya mgongano wa
nadharia zinazojirudia zinazothibitishwa tu na mfululizo wa visa.
Hapa, ninatoa uthibitisho kwamba uchumi huru unachangia kushuka kwa migogoro miongoni mwa nchi. Kwanza, hata hivyo, ninahitaji kuufanya kuwa wa kisasa mtazamo wa vita wa siasa – uchumi wa jadi. Mapokeo ya amani ya kibepari ni tajiri lakini wenye msingi mbovu katika utambuzi muhimu kuhusu kwa nini nchi zinapigana. Uelewa
kuhusu kwa nini nchi zinapigana. Uelewa mzuri wa jinsi masoko huria
yanavyookoa nchi huru kuhusu umuhimu wa kufanya vita unaweza kusaidia
kuimarisha na ikiwezekana kuendeleza amani miongoni mwa nchi za
kibepari zilizoendelea.
Uhuru wa Kiuchumi na Vita vya Dunia
Norman
Angell (1933), mfuasi mkubwa wa shule yenye mtazamo usiojifunga na
iliyopata Tuzo ya Amani ya Nobeli kwa kazi ya uandishi na mwanasias. Anabainisha michakato miwili inayokusudiwa kupunguza maombi ya uvamizi miongoni mwa nchi zilizoendelea. Kwanza, maendeleo yanapelekea kwenye mabadiliko katika uzalishaji ambayo yanafanya mashambulizi na uvamizi visiwe na faida.
Wakati wa robo ya mwisho ya karne ya kumi, Anlaf the Viking
alikuja mara tatu Essex – na kila safari alifanya kitu kizuri: meli
zake, kwa idadi 90, zilizotolewa kwenye mlango mpana zilizosheheni
mahindi, na ngozi za wanyama, na nguo nzuri kutoka kwenye nyumba za
watawa…. Mtiifu kwa amri ya kukumbuka kwamba nguvu zilizoko nyuma
hazijabadilika, nimejaribu kuwafikiria Waingereza, sasa kwa kuwa hivi
sasa wana udhibiti mkamilifu, kurudisha ukamilifu karne kumi baadaye:
wanamaji wetu wakipakia sehemu nzuri ya mali zetu za biashara kwa
utajiri wa bidhaa za kilimo na viwanda za rasi ya Scandinavia (Angell,
1933: 103).
Hakika, ilikuwa inaonekana kama upumbavu kumfikiria mwanamaji Mwingereza kama Marauding Vikings. Mambo yalikuwa yamebadilika ilipofikia karne ya ishirini na bado ndani ya mwongo wa uchapishaji wa toleo la pili la The Great Illusion,
Uingereza ililinda Iceland¹ na karibu ivamie Norway (Kersaudy, 1990)²,
Ujerumani ilikalia Denmark na Norway (Ziemke, 1990), na Finland
iliingizwa kwenye vita na Urusi (Engle na wenzake, 1992). Sweden pekee
ilibakia na uhuru wake na kutokufungamana na upande wowote.
Inachukua juhudi kidogo tu kuwafikiria Hitler, Massolini, na Tojo katika dhima ya Vikings. Nguvu
za mhimili zilichangia itikadi ambayo ilikuwa na kumbukumbu wakati
ambao uhimizaji wa nguvu za nchi, ulimaanisha upanuaji wa eneo
(Weinberg, 1994; Cassels, 2003)3 Bado, wakati
Vita Kuu vya Pili ya Dunia vingeweza kuonekana kama “jambo baya zaidi”,
inawezekana kuhoji kwamba maendeleo yanazuia migogoro katika matukio
fulani. Tangu mwanzo, malengo ya awali ya mihimili ya nchi yalikuwa nchi maskini kuhusu ukingo wa uchumi wa Ulaya. Vita
na Ulaya Magharibi ilifikiriwa kwa sababu za kimkakati, kuzitisha
Ufaransa na Uingereza, zisichukue raslimali (Weimberg, 1994). Kwa
nini Hitler – mfano wa kila mtu wa ukatili – alifuatilia majimbo
maskini ya Ulaya Mashariki wakati nchi nyingi tajiri za Ulaya zilikuwa
Magharibi? Isipokuwa Finland, hakuna nchi za Kiskandinavia
zilizoshambuliwa kwa lengo la kupanua eneo. Uvamizi wa Ujerumani katika nchi ya Norway ulikusudiwa kwanza kwa ajili ya kuzuia uvamizi wa Uingereza (Ziemke, 1990). Miongoni
mwa wapiganaji wakubwa hakuna yeyote aliyesukumwa na shauku ya kuteka
Norway au kupata eneo la nyongeza au raslimali kwa nguvu. Uvamizi uliopangwa wa Uingereza – Ufaransa ulikusudiwa kulinda njia za meli za kaskazini na malengo ambayo yalikuwa na maana kufanya vita kubwa. Hakika, hali ya Norway kutokufungamana na yeyote ilielekea kukamilisha malengo ya Ujerumani4. Hitler
hajawahi kushambulia Sweden yenye utajiri mkubwa na chanzo kikubwa cha
Wajerumani cha mawe yenye madini ya chuma, ambayo nusu yake
ilisafirishwa kupitia Norway (Fox, 1959; Hägglöf, 1960)5. Hata
baada ya marafiki kushindwa kuingilia kati, Ujerumani ilipendelea
kununua, kuliko kuchukua kwa kutumia nguvu, mali nyingi ya rasi ya
Scandinavia6.
Hii haimaanishi kwamba Sweden haikuathiriwa na vita. Maofisa
wa Nazi walitumia kutokulingana huko katika nguvu kuishinikiza serikali
ya Sweden kuhusu masuala mbalimbali, hususan upitishaji wa vifaa na
wafanyakazi kupitia nchi ambayo haifungamani na yoyote. Sweden
ilibakia huru kwa kuwa ilizalisha zaidi kupeleka Axis kwa kutumia
biashara kuliko uvamizi na kwa sababu iliamuliwa kwa busara kuegemea
kidiplomasia pale ambapo Norway iliacha (Carlgren, 1977)7. Bado, Ujerumani ilichagua kutokuvamia Sweden wakati ingeweza kufanya hivyo kwa urahisi. Uwezo
wa kujizuia wa Hitler kwa kiasi kidogo sana ulisababishwa na upinzani
au vikwazo vya kimaadili katika kutumia nguvu ya uhuru. Badala
yake inaonyesha kuwa makisio mepesi kung’amua hayo yalifanywa kwamba
ilikuwa rahisi kufanya biashara kuliko kuchukua raslimali
zilizohitajika za Sweden.
Mchakato wa pili Angell anaouonyesha unahusisha ulegezaji wa masharti ya kiuchumi. Kuongezeka
kwa ushirikiano wa masoko ya dunia kunarahisisha upataji wa bidhaa na
huduma kupitia biashara na ugumu kuepuka wawekezaji wasio na utulivu
katika vita. Angell anafikiria Jeshi la uvamizi la Ujerumani mjini London.
Pamoja
na manufaa ambayo Ujerumani ingeweza kupata kwa kushikilia dhahabu ya
Uingereza, hakika, ingekuwa zaidi ya fidia kwa ukweli kwamba lilikuwa
tendo la kikatili la serikali ya Wajerumani ambalo limesababisha balaa
kubwa. Nchi ambayo ingeweza kupora akiba ya benki ingefaa
kuepukwa na wawekezaji: umuhimu wa mkopo ni imani, na wale ambao
wanakataa kuulipa wanalipia vitendo vyao. Jemadari mkuu wa majeshi yote ya Kijerumani mjini London anaweza asiwe na ustaarabu zaidi ya Anlaf mwenyewe, lakini karibuni angeona tofauti baina yake na Anlaf. Anlaf
hakupaswa kuona shaka kuhusu kiwango cha benki na matatizo kama hayo;
lakini Generali wa Kijerumani, akijaribu kupora Benki ya Uingereza,
anaweza kukuta salio lake mwenyewe kwenye Benki ya Ujerumani
limetoweka, na thamani ya hata sehemu kubwa ya vitega uchumi vyake
imepungua. (Angell, 1933:106-07).
Kwa mara nyingine tena Angell ameonekana kukosea, labda mtu aangalie kwa karibu sana. Mara
kwa mara, inakumbukwa kwamba Vita Kuu vya Kwanza vya Dunia vilianzia
Balkans lakini kwa ujumla inasahaulika kwamba Balkans ilikuwa sehemu
iliyokuwa ya nyuma sana kiuchumi katika Ulaya. Wakati
vita haikuwepo katika mfululizo wa migogoro miongoni mwa mataifa
makubwa ya Magharibi yaliyotegemeana kiuchumi hadi 1914, migogoro
katika Balkans kila wakati ilipelekea kwenye vita (Strachan, 2001). Hivyo, mgogoro katika Balkans ni rahisi kuielezea kwa kuangalia uhuru wa kiuchumi. Mashindano
ya ndani yaliyoanzishwa na Austria – Hungary dhidi ya Serbia yalienea
katika mfumo mkubwa wa ushirikiano wa marafiki (Kissinger, 1994)8. Tatizo
la Ulaya kwa 1914 lilikuwa hasa kwamba ulegezaji masharti ya uchumi na
ushirikiano wa kiuchumi havikuwa sawa, wakati wajibu wa kisiasa
ulihakikisha kuwa kutegemeana kiuchumi huko Magharibi hakukuwa na maana
tena. Mataifa yaliyoendelea sana yalifanya sera zao za
nje kuwaza kibalkan ili kuongeza nguvu ya ushawishi ya kujadiliana
malipo ya mataifa yenye nguvu ya Ulaya Mashariki. Kwa
kiwango kwamba uhusiano wa kirafiki uliheshimiwa, maamuzi ya
uhamasishaji yalikuwa mikononi mwa nchi hizo ambazo hazikutegemea
vizuizi vya kiuchumi ambavyo Angell alielezea kwa ushawishi mkubwa.
Kushindwa
kutegemeana kiuchumi katika kuzuia uenezaji wa mawazo potofu ya vita
hakumaanishi kutokufaa katika kuzuia cheche za awali. Kushindwa kutabiri vita ya dunia kulifunika ukweli muhimu wa madai ya Angell. Matukio yaliyofuatia vita yalionekana kulingana na dira ya Anglii ya amani isiyo na upendeleo. Uchumi wa sasa hauonekani kama unaongozwa na uvamizi wa kijeshi (Brooks, 1999)9. Hivyo, kosa la Angell ni kwamba anatoa dhana finyu kupita kiasi ya sababu za mgogoro kati ya nchi na nchi. Nchi zinashindana, sio kwa ajili ya raslimali, bali juu ya sera na jiografia mkakati. Mtu anapokaa kwenye ramani ina maana maalum, hususan kama yuko baina ya wahusika wakuu katika migogoro (Fazal, 2002). Vivyo
hivyo kinachotakiwa na nchi, bila kutegemea thamani ya maeneo au
raslimali zake, kinaelekea kuvuta vivutio vya wengine ili kulaumu au
kuzipeleka vitani (Maravcsik, 1997). Hivyo, amani ya kibepari inayoahidiwa na Angell na kundi lingine la kimapokeo sio mbaya bali haijakamilika. Maelezo
kama yalivyoendelezwa yana utambuzi muhimu kwamba, mara yatakapopitiwa,
yatathibitisha kwamba ni nadharia jarabati, halali
Amani ya Kibepari
Maelezo Yanayoendelea
Katika Msimamo wa Kisheria,
Montesquieu anasema kwamba “Mfanyabiashara tajiri sana alikuwa tu na
mali isiyoonekana ambayo ingeweza kupelekewa kila mahali bila ya kuacha
hata kiasi kidogo… [ili] watawala wamelazimika kutawala kwa hekima
nyingi sana kuliko ambavyo wenyewe wangeweza kufikiri” (1989 [1748]:
389). Uhuru wa kiuchumi maana yake unaweza ukauchukua. Wakati hali ikiwa mbaya ndani, mtaji huweza kuondoka nchini, na kutengeneza ukame kiuchumi na hivyo kisiasa katika jamii. Ni wazi kwamba, serikali hazitaki fedha zitoke. Kwa
kiwango ambacho watawala hawawezi kuzuia kuondoka kwa mtaji, hata
hivyo, lazima watengeneze mazingira yatakayosaidia uwekaji wa fedha kwa
hiari ndani ya mipaka yao.
Utamaduni
wa wasomi wanaopenda mabadiliko ya amani katika uchumi yaliyoanza na
Montesqueieu, Mill, Adam Smith, na wengine, na kuendelea hadi kwa
Richard Cobden, Norman Angell, na Richard Rosecrance inaweza kuhimiza
amani. Labda maelezo ya jumla zaidi ni kwamba kutegemeana kiuchumi
kunaweza kuleta kitu cha thamani ya pamoja kwa nchi, kuziacha nchi
kukataa kufanya kitu kupambana kwa ajili ya hofu ya kuharibu manufaa ya uchumi wanaouthamini sana. Wakati
haya ni kweli, maelezo yanategemea kufikiria kwamba vipengele vya
thamani ya pamoja vyenyewe havianzishi wala kuwezesha mgogoro. Thomas
Schelling anaeleza hadithi ya wapanda mlima wawili waliofungwa pamoja
na kamba ambayo husababisha pamoja na kamba ambayo husababisha waelekee
sehemu moja. Schelling anaonyesha namna kitu chenye
thamani kwa wote kinavyoweza kutumika kimkakati kumtawala mwenzie; nchi
ambazo zina ushirikiano wa kiuchumi zinaweza kucheza mchezo wa kuku:
uhusiano ulivyo mkubwa sana, mchezo ndio unafanikiwa na kuelezeka
(Schelling, 1966: 99-100). Kama nchi inasita kuhatarisha faida za uhusiano wa uchumi unaostawi, sio kwamba amani itafuatia. Nchi nyingine zinaweza kushawishika kutazama usitaji wa kupigana kama kuweza kudhuriwa. Ili kuhakikisha kuna amani, washiriki wote lazima wasiwe tayari kucheza mchezo wa kuku au, hakika, kutumia nguvu za kijeshi.
Zamani wanafunzi wa ushirikiano wa kimataifa waliangalia sababu na fursa za kuelezea vita. Hata
hivyo, kama ilivyo kwa vitabu vya hadithi za mauaji ya siri na mchezo
wa Clue unaoweka wazi, masharti haya mara chache hutosha. Watu
binafsi, vikundi, na nchi mara nyingi zinakataa, bali kwa kawaida
vyombo vyenye raghaba tofauti vinajikuta vinaweza kujadiliana bei
ambazo zinaweza kuepuka gharama zaidi au tabia za ushaufu. Nini sasa kinachoelezea kufanikiwa au kushindwa kidiplomasia? Mojawapo ya matatizo ya msingi katika ushirikiano wa kimataifa – ni kufahamu wakati mpinzani anapokuwa anasema au hasemi ukweli. Viongozi wakati wote watadai kuwa tayari kutumia nguvu wakati ukweli ni kwamba wanadanganya. Vita
hutokana na sababu kadhaa lakini kinachochangia hasa ni kutokuwa na
uhakika kuhusu mapatano ya dau ambalo lingekubaliwa na mpinzani. Kama
mtu anakubali kuwa vita ni mbinu ambayo ina gharama kubwa ya kuamua
umiliki wa raslimali au haki za sera, kisha ziada inayotokana na
ufumbuzi wa kidiplomasia inapaswa kufanya majadiliano ya kupatana bei
kupendelea kupigana10. Kama wachezaji wa poka
wanavyolinda kazi zao, uongozi wa kisiasa wa mataifa unaona kwamba
wakati mwingine unapaswa kudanganya ili kushinda. Kwa kutokuwa na uhakika na vichocheo vya kudanganya, hata hivyo, diplomasia inaweza kushindwa na migogoro kuzuka. Baada
ya hapo vita hufichua maelezo kuhusu “kadi” zilizoshikiliwa na
wapiganaji husika (taarifa kuhusu uwezo wianifu wa nchi na ufumbuzi). Kwa
hakika, ili vita ikome, pande husika katika mashindano lazima zijifunze
kwa kiasi cha kutosha kufanya mapatano kuhusu majadiliano ya malipo ya
pamoja yaliyokubalika. Uhuru wa kiuchumi ni muhimu kwa amani kwa angalau sababu mbili. Kwanza, masoko huria hufanya kazi kama njia ya kuenezea maoni kwa ajili ya shughuli za kisiasa. Vitendo
vinavyotishia masoko vinapinga uwekezaji, kushusha chini masharti ya
uchumi wa ndani, na hivyo yanaelekea kuepukwa na viongozi wa ndani. Utumiaji
wa nguvu ng’ambo mara nyingi unahusishwa na kushuka kwa uwekezaji wa
ndani na mbubujiko wa mtaji (Bueno de Mesquita, 1990). Kwa
kiwango kwamba viongozi wako tayari kutoa matamko ya sera ya nje ambayo
yanatishia masoko ya mtaji, na kwa kiasi kwamba sera hizo huru za fedha
zipo ambazo zinaleta ugumu kwa serikali kuingilia mtiririko wa mtaji,
jumuiya ya kimataifa inaweza kuona azma ya kweli ya viongozi. Kwa
kujua kile ambacho mpinzani yuko tayari kufanya kunasaidia kujadili
malipo kwa ufanisi zaidi, ili kwamba kukimbilia kufanya vurugu ili
kupata kile ambacho upande mmoja unahitaji mara nyingi sio lazima sana. Masoko huru ya kuleta kuaminika bila ya kuhitaji kushadidia nguvu ya kijeshi (Gartzke na wenzake, 2001; Gartzke & Li, 2003).
Jedwali la 2.1 linabainisha viukilia vya migogoro ya kijeshi kati ya nchi na nchi (MIDS),
inayoelezewa kama tishio kubwa sana au utumiaji mkubwa wa nguvu, hadi
kufikia na kujumuisha vita vinavyohusisha vifo 1000 kwenye uwanja wa
vita. MIDS ni kiashirio kikubwa cha tabia ya
migogoro kinachotumiwa na watafiti katika ushirikiano wa kimataifa
(Gochman na Maoz, 1984, n.k) yamewekwa alama ya “1” kama kuna mgogoro
katika mwaka huo unaohusu nchi na “0” vinginevyo. Uchambuzi
wa kurudi nyuma unaleta kizigeu kati ya vipimo viwili kwa kila chenye
kubadilikabadilika, ambao unaonyesha ukubwa wa athari wa kitu hicho
kinachobadilikabadilika kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa MID hapo kwa
mwaka husika, kwa kuzingatia athari ya vitu vingine
vinavyobadilikabadilika. Mkadiriaji wa kurudi nyuma pia anaonyesha jinsi mtu anavyopaswa kujiamini katika kizigeu wiano kilichokadiriwa. Matukio
ya kijamii kwa kawaida huonekana kama yenye welekeo: hata wakati
vipengele vyote muhimu vinavyochangia vinafanana, matokeo yanaweza
kutofautiana kutoka jambo hadi jambo. Labda uhusiano ulio dhahiri baina ya kitu huru kinachobadilikabadilika na migogoro ni dhahiri tu. Mfano
wa kurudi nyuma unashughulikia tatizo hili kwa kuanzisha safu au
mgawanyo wa uhusiano unaowezekana baina ya chanzo na athari. Kosa kubwa linaonyesha “kuenea” kwa mgawanyo huu wa kizigeu kinachowezekana. Kama
kosa ni kubwa likilinganishwa na kizigeu (takribani, kubwa zaidi ya
nusu ya ukubwa wa kizigeu), basi inawezekana kuwa kizigeu halisi
kinachozalisha data ni sawa na ziro na kwamba hakuna uhusiano uliopo
baina ya kitu kinachobadilikabadilika na iwapo nchi zinapigana. Kipimo
cha “umuhimu wa kitakwimu” kinachonyesha kitu ambacho tungeweza
kukubali bila usahihi wa kizigeu kama kinavyoonyesha uhusiano baina ya
chanzo na sababu. Ubadilishaji ni kutumia kiwango muhimu cha juu cha 1%, 5%, au 10%. Ili
kukubali uhusiano, tunahitaji kwamba kati ya majaribio 100 yenye data
zinazolingana, kati ya 90 na 99 ya makadirio ya kizigeu kilichotolewa
ziwe tofauti kutoka ziro13.
Jedwali la 2.1 Athari ya Uhuru wa Kiuchumi kwenye Migogoro ya Kijeshi Kati ya Nchi (MIDs)
Nyanja
Uhuru wa kiuchumi -0.567**
Uwezo
Idadi ya watu 2.08×10-6* (8.18×10-7)
Nguvu kubwa? 0.853
Alama za Demokrasia -0.628
Mkataba wa ulinzi? -0.011
GDP kwa kila mtu
Uwazi wa Biashara 1.57×10-7
– Spline 1
– Spline 2
– Spline 3
Kuingilia kati -0.381
N
Log – Likelihood
X2(II)
Viwango muhimu +: 10% *:5% **:1%
Mkabala
huu unathibitisha kwamba dunia ina mshindo mkubwa (“stochastic”) wakati
huohuo kupunguza hatari ya kukubali nadharia ambazo kwa hakika ni za
uongo.
Chanzo kikuu au vitu “pekee” vinavyobadilikabadilika katika uchambuzi ni uhuru wa kiuchumi. Hiki ni kielelezo kilichotengenezwa na Gwartney, Lowason na wengineo kupima msimamo wa kupendelea mabadiliko wa uchumi wa nchi. Kama inavyoweza kuonekana katika Jedwali la 2.1, uhuru wa kiuchumi kipekee hupunguza uwezekano wa nchi kuwa na mgogoro14. Vipo
vipengele vingine kadhaa vinavyobadilikabadilika vilivyoingizwa kwenye
uchambuzi ili kuhakikisha kuwa matokeo kwa ajili ya uhuru wa kiuchumi
sio ya uwongo. Vipengele hivi vyote vinavyobadilikabadilika ni vya kawaida sana katika utafiti wa kiasi wa migogoro ya kimataifa. uwezo
unajaribu kushika dhana ya “nguvu” kwa kuripoti asilimia ya wastani ya
uwezo wa jumla wa dunia mbao taifa linaweza kuwa nao katika makundi
sita yanayoonyesha vipengele vinavyobadilikabadilika vya kijeshi,
kiuchumi na kidemografia. Nchi kubwa na zenye nguvu zinaelekea kuwa na migogoro zaidi kuliko zile ndogo. Idadi ya watu inaripoti jumla ya idadi ya watu wazima kwa nchi. Alama ya Demokrasia ni kiashirio cha kiasi cha “udemokrasia” cha nchi. Nguvu kubwa? Na Mkataba wa Ulinzi? Ni
vipengele vinavyobadilikabadilika vya mwainisho wenye upinzani (mwigo)
vilivyopewa alama “1” kama nchi husika ni nguvu kubwa au kama nchi ina
urafiki mkubwa kijeshi na nchi nyingine ambayo inaweza kuusaidia wakati
wa vita. Pata Ghafi la Taifa kwa kila mtu linapima wastani wa pato la taifa nchini. Hili
ni muhimu kujumuisha, kwa kuwa tunatafuta kujua kama ni ustawi wenyewe
au kwa ufinyu ziadi uhuru wa kiuchumi ambao uHoja za Uongobisha amani. Vivyo hivyo, Uwazi wa Biashara unaweza kuwa ni kitu kingine kinachozuia migogoro. Mwishowe,
ninajumuisha idadi ya vipengele vinavyobadilikabadilika ambavyo
vinashughulikia tatizo la kiutaalamu linalotokea wakati tabia ya vita
inahusishwa na jinsi wakati unavyokwenda. Mbinu ya ukadiriaji hudhania kwamba migogoro haihusiani. Ni wazi, mgogoro katika mwaka husika unaweza kuenea na kuchangia kwa mingine inayofuatia. Kuongoza vipengele vinavyobadilikabadilika vya spline kunahakikisha kwamba matokeo hayatokani na chanzo cha usababisho15.
Mbele ya vipengele vinavyobadilikabadilika vya spline, ni Uhuru wa Kiuchumi tu na, pili, idadi ya watu ndiyo muhimu kitakwimu. Muundo wa uchumi na kwa kiwango fulani ukubwa wa kidemografia huathiri migogoro lakini hatuwezi kutumaini kwamba vipengele vingine vinavyobadilikabadilika vina athari kuhusu kama nchi inapigana.
Wakati
mtu anaweza kuangalia kizigeu na makosa ya kiasi kwenye Jedwali la 2.1
na haraka kuamua iwapo uhusiano unaodaiwa unafaa kukubaliwa (au
usikataliwe), ni rahisi kidogo kuamua ni kiasi gani kipengele
kinachobadilikabadilika kinafaa kama nchi zinapigana. Kurudi
nyuma kilogitii kunaruhusu watafiti kuchunguza hali iwapo matokeo ya
raghaba ni ya mwainisho wenye ukinzani (k.v. “vita”, “hakuna vita”). Hata
hivyo, kwa sababu za kiufundi, mkadiriaji wa kurudi nyuma lazima
ayashughulikie matokeo kama vile yalikuwa yanaendelea (k.v. kwa kadri
ya kitu, kama vile kukadiria ukubwa au uelekeo wa mgogoro), Badala
ya kutabiri kuwepo kwa mgogoro au kutokuwepo kwa mgogoro, kisha,
mkadiriaji wa logiti anatabiri uelekeo wa kuwepo na ugomvi. Ili kuhakikisha kuna raslimali nzuri kwa ajili ya uelekeo uliotabiriwa, logiti inatumia uwiano unaohusu batli asilia16. Kama
vile kubadilisha viwango vya desimali kwa mfumo wa alama wa jozi ili
kuviruhusu vitathminiwe na kompyuta, kigeuzi cha logi kinawezesha
makadirio na majaribio muhimu kwa kiasi cha gharama ya kuhisi. Vizigeu vinavyotokea vinafafanuliwa vizuri zaidi kwa uwekaji uelekeo uliotabiriwa unaokadiriwa na kurudi nyuma kwa logiti.
Athari
halisi za Uhuru wa Kiuchumi na Alama za Kidemokrasia kuhusiana na
migogoro ya kimataifa zinaweza kuonekana katika mchoro 2.1 na 2.2,
mtawalia. Katika michoro yote miwili, mhimili wa mlalo
unaorodhesha vipimo vya mpango kwa ajili ya vipengele husika
vinavyobadilikabadilika (ama Kielelezo cha Uhuru wa Kiuchumi au
kielelezo cha serikali ya Kidemokrasia), wakati mhimili wa wima
unaripoti uelekeo wa MID katika mwaka husika kwa nchi zenye kiwango cha
mojawapo ya vipengele viwili vinavyobadilikabadilika vinavyojieleza. Mstari
mnene unaoinama chini kuelekea kulia katika Mchoro wa 2.1 ni uhusiano
baina ya Uhuru wa Kiuchumi na migogoro ya kijeshi, kama ilivyokadiriwa
kwa kurudi nyuma katika Jedwali la 2.1. Katika Mchoro wa
2.2, athari ya Kipengele kinachobadilikabadilika cha Alama ya
Kidemokrasia kuhusu mgogoro huonyesha pia kama mstari mnene, unaoinama
chini kidogo na kuelekea kulia. Katika mchoro wa 2.1,
mistari miwili ya dashi hafifu ambayo inaonekana kwenda uhuru wa
kiuichumi inawakilisha vipindi vya kujiamini. Asilimia
tisini na tano ya mistari yote minene iliyokadiriwa kutoka kurudi nyuma
kwa data zinazofanana ingekuwemo ndani ya kipindi kilichopakana na
mistari miwili yenye dashi. Kwa maneno mengine, uhusiano
ulioonyeshwa katika mchoro baina ya Uhuru wa Kiuchumi na kutokuwepo na
vurugu za kijeshi unaelekea angalau kuwa sahihi.
Kama inavyoweza kuonekana katika serikali yenye upungufu ni makubwa. Nchi huru ndogo zaidi zina karibu
nafasi ya 7% ya kuwa na migogoro, wakati nchi zilizo huru zaidi huwa na
migogoro kwa karibu nusu tu ya 1% ya mwaka uliochunguzwa. Kuufanya uchumi kuwa huru zaidi maana yake ni kuzifanya nchi kuwa na amani zaidi. Kwa kuzidi sana, nchi zilizo huru kidogo ni karibu mara 14 kuwa na migogoro kama zilizo huru zaidi.
Hayohayo hayawezi kusemwa kwa uhusiano baina ya demokrasia na mgogoro. Nafasi
ya mlalo ya mstari katika Mchoro 2.2 inaonyesha kuwa kipengele
kinachobadilikabadilika cha Alama ya Kidemokrasia hakina athari kwa
migogoro ya kijeshi.17 Nchi zenye demokrasia ndogo (karibu ziro) na zenye demokrasia kubwa (karibu 10) zinaelekea zaidi kuwa na migogoro. Ukweli
ni kwamba, mlingano wa kiwango cha kuzidi sana wa Uhuru wa Kiuchumi wa
Alama ya Kidemokrasia unaonyesha kwamba aliyetangulia ana takriban mara
54 zaidi ya athari kuhusu tabia ya mgogoro kama wa kwanza.
Mchoro wa 2.1: Athari ya Uhuru wa Kiuchumi kuhusu Migogoro ya Kijeshi Kati ya nchi na nchi (MIDs)
0.10
0.08
0.06
0.04
0.02
Huru kidogo 3 4 5 6 7 8 Huru zaidi
Chanzo: Jedwal
Mchoro wa 2.2: Athari ya Demokrasia Kuhusu Migogoro ya Kijeshi Kati ya Nchi na Nchi (MIDs)
0.10
0.08
0.06
0.04
0.02
Udikteta 2 4 6 8
Wala
mtu asichukue ukweli kwamba mstari wa Alama za Kidemokrasia ni karibu
na Ziro kama ishara kwamba vita haviwezi kutokea katika demokrasia. Uamuzi hutegemea mabadiliko ya pande zote. Bila
ya kujali kama mbinu ni za asili (za majaribio), kinadharia, au
kitakwimu, mtu “anatafutiza” chanzo na kutazama mwendo unaohusiana
katika kipengele kinachobadilikabadilika cha matokeo. Hapa hakuna mwendo katika matokeo; demokrasia haiathiri welekeo wa MIDs. Ukweli kwamba viwango vya juu vya kipengele kinachobadilikabadilika cha Alama za Kidemokrasia kinaongeza migogoro. Mstari
wa mbele juu ya ule wa chini katika Mchoro 2.2, mstari wa dashi hafifu
kwa kipindi cha juu cha imani, uhusiano uliokadiriwa katika data
zinazofanana vitatoa ripoti kwamba demokrasia hufanya migogoro iweze
kuwepo.
Vipengele vya ziada vinavyozingatiwa
Vipengele
viwili vya uthibitisho vimetumika kuelezea amani katika zama za sasa
ambavyo havikujumuishwa kwenye uchambuzi katika Jedwali 2.1. Kwanza,
baadhi ya nchi zimo kwenye mipangilio ya pamoja ya usalama au
mipangilio ya biashara ya kanda ambayo inaweza kupunguza tabia ya
kupigana wenyewe kwa wenyewe. Umoja wa Ulaya (EU) labda
ni mfano bora zaidi wa jumuiya ya mataifa ambayo inafikiriwa kubadili
vita kwa mafanikio kwa mwingiliano wa amani. Sababu zinatofautiana bali wengi wamedai kwamba asasi na utamaduni wa EU vinahimiza fikra na kuzuia vurugu miongoni mwa wanachama. Pili, watafiti kama vile Kenneth Waltz na John Mearsheimer wanasisitiza kwamba silaha za nyuklia zinaweza kuwa kama kizuizi. Nchi zinaweza kusita kupigana na nchi zenye silaha za nyuklia. Ili
ujaribu vipengele hivi vinavyowezekana vya kustaajabisha sana,
ninaongeza vipengele viwili vinavyobadilikabadilika ambavyo vinapima
uanachama katika Jumuiya ya Ulaya na umiliki wa silaha za nyuklia
katika Jedwali la 2.2. Mwanachama wa EU? ni kipengele kinachobadilikabadilika mwigo sawa na “1” kama nchi ni mwanachama wa Jumuiya ya Ulaya katika mwaka husika. Vivyo hivyo, Silaha za Nyuklia? hubainisha zile nchi zilizomiliki, au ambazo ziliaminika pote kwamba zilimiliki, silaha za nyuklia katika mwaka husika. Wala
kipengele kinachobadilikabadilika hakitabadilisha kwa kiasi kikubwa
welekeo kwamba nchi itahusika katika mgogoro wa kijeshi. Zaidi ya hayo, uhuru wa kiuchumi unabakia kuwa mtabiri muhimu kitakwimu wa tabia ya migogoro.
Ni muhimu kuhakikisha kwamba matokeo yaliyoripotiwa hapa hayatokani na kosa au mawazo ya kutamani. Uchunguzi
wa maelezo mbadala yanayowezekana yasingeonekana kikamilifu kama
tungepuuza vipengele vinavyobadilikabadilika vya kidemografia. Vipengele vya kidemografia vinavyowezekana ni vingi. Nimechunguza
vingi lakini nitatoa mifano michache tu katika Jedwali la 2.3. Eneo la
Ardhi la Jumla linaripoti idadi ya hektari za ardhi lililozungukwa na
mipaka ya nchi. Kijiografia nchi kubwa sana, bila ya
kuangalia idadi ya watu, zinaweza kufanya mambo tofauti na nchi ndogo,
ambazo nyingi hutegemea biashara zaidi. Inawezekana pia kwamba nchi zenye watu wengi sana huwa na migogoro sana. Msongamano
wa idadi ya watu unaonyesha idadi ya watu wazima kwa hektari,
yawezekana unaakisi “Shinikizo la pembeni” (Choucri na North, 1975,
1989). Idadi ya Nchi Enezi zinaonyesha iwapo nchi ina majirani wengi na kwa hiyo kuwa na uwezekano wa migogoro mingi. Hatimaye,
Ardhi Inayolimika/Idadi ya Watu inatofautisha nchi zenye maeneo makubwa
ya makazi na malisho na zile zenye ardhi kubwa ya kilimo. Kama
mwanzo, hakuna badiliko katika matokeo kwa kipingele
kinachobadilikabadilika cha Uhuru wa Kiuchumi na hakuna kimojawapo kati
ya vipengele vinavyobadilikabadilika vipya ni muhimu kitakwimu.
Jaribio la mwisho la nguvu linahusisha kugawa sampuli ya nchi kwa kanda. Utafiti wa hivi karibu wa ushirikiano wa kimataifa umesisitiza umuhimu wa utofauti wa kanda. Tabia
ya migogoro ya nchi za Afrika husababishwa kwa sehemu na vipengele
tofauti na vile vinavyosababisha tabia za migogoro huko Ulaya au
Amerika Kaskazini. Ili kushughulikia uwezekano kwamba matokeo ya Uhuru wa Kiuchumi yanaweza kuakisi tofauti za kikanda, ninajumuisha seti ya vipengele vinavyobadilikabadilika mwigo katika kanda. Vipengele hivi vinavyobadilikabadilika vilivyowekwa alama kwa ajili ya kanda husika18 vimeongezwa kwenye Jedwali la 2.4. Baadhi
ya miigo ya kikanda ni muhimu kitakwimu, kuonyesha kwamba vyanzo vya
migogoro hutofautiana katika sehemu tofauti za dunia. Hata hivyo, Uhuru wa kiuchumi hausumbuliwi na kuwepo kwa kanda mbalimbali. Matokeo yanaonyesha uhusiano mkubwa zaidi baina ya masoko huria na amani. Hakika
uhuru wa kiuchumi ni kipengele pekee kinachobadilikabadilika ambacho
kinathibitisha ulinganifu kitakwimu na kiumuhimu katika michanganuo
hii.
Mustakabali wa Amani ya Kibepari
Matokeo yaliyoripotiwa hapo juu yanawezesha kubahatisha kuhusu kuanza kwa ushirikiano wa kimataifa. Baadhi ya vidokezi vinaleta matumaini na baadhi havileti. Nchi
zenye uchumi huria na unaostawi zina nafasi nzuri ya kudumisha na hata
kuzidisha amani ambayo ilikuwepo kwa iliyotangulia kwa nusu ya karne ya
ishirini kuhama.
Jedwali la 2.2: Kuongeza Uanachama katika EU na Umiliki wa Silaha za nyuklia
Kipengele kinachobadilika Kizigeu (Kosa kiasi) Badilika
______________________________ Uhuru wa kiuchumi -0.531** (0.176)
Uwezo Idadi ya watu 1.68×10-6* (9.74×10-7) Nguvu kubwa? 0.452 (1.130) Alama ya Demokrasia -0.030 (0.065) Mkataba wa ulinzi? -0.472 (0.560) GDP kwa kila mtu 2.95×10-6 (8.14×10-5) Uwazi wa Biashara 4.43×10-7 (1.46×10-6) Uanachama wa EU? -0.865 (0.865) Silaha ya Nyuklia? 1.321 (1.014) – Spline 1 6.16×10-4** (2.35×10-4) – Spline 2 -4.62×10-4** (1.77×10-4) – Spline 3 1.23×10-4* (4.8×10-5) Muingiliano -0.562 (1.341)
______________________________
______________________________
N Log – Likelihood -159.49
X2(I3) Viwango vyenye umuhimu +: 10% *:5% **:1%.
______________________________
|
Jedwali la 2.3 Uchunguzi wa sababu za ziada za
Kidemografia
Nyanja
______________________________
Uhuru wa kiuchumi -0.779** (0.221)
Uwezo
Idadi ya watu 2.27×10-6* (1.14×10-6)
Taifa kubwa? 1.148 (0.969)
Alama za Demokrasia -0.008 (0.0659)
Maafikiano ya Ulinzi? -0.536 (0.462)
GDP kwa kila mtu 1.12×10-5 (6.63×10-5)
Uwazi wa Kibiashara 5.03×10-8 (1.50×10-6)
Jumla ya Eneo la Ardhi 8.74×10-8 (1.69×10-7)
Wingi wa watu 2.87×10-4 (2.42×10-4)
Idadi ya Nchi za Jirani -0.157 (0.097)
Ardhi inayolimika/idadi ya watu -0.23 (0.111)
– Spline 1